Wahusika Wamisri

“Mohamed Metwally Al- Shaarawi”

Mwanachuni wa Dini , waziri wa zamani wa masuala ya kidini (Awqaf).

ni mmoja wa wafsiri wa maarufu sana wa Qur’an katika zama za kisasa.Alifanya kazi katika kutafsiri Qur’ani Tukufu kwa njia rahisi na mazungumzo ya kawaida , ambayo iliwezesha kufikia sehemu kubwa ya Waislamu katika ulimwengu wa Kiarabu. Wengine waliitwa Imamu wa wahubiri.

Kuzaliwa na maisha ya kisayansi

Alizaliwa katika  tarehe 15 mwezi wa Aprili, mwaka wa 1911 katika kijiji cha Daqados, mji wa Met Ghamr,  Mkoa wa Dakahlia huko Misri, na alihifadhi Qurani  tukufu akiwa na umri wa kumi na moja , Alipata shuhuda ya msingi ya Al-Azhar mwaka wa 1923 na akaingia shule ya sekondari ya Al-Azhar, Na kuongezeka  uelekevu wake kwa Ushairi na fasihi . , Na alipata nafasi maalum kati ya wenzake, wakamchagua kuwa Rais wa Umoja wa Wanafunzi, na Rais wa Chama cha Waandishi  huko Zagazig, kisha akajiunga na Kitivo cha lugha ya Kiarabu, Chuo Kikuu cha Al-Azhar mwaka wa 1937, Alihitimu masomo yake mwaka wa 1940. Alipata daraja za kimataifa na shuhuda ya kufundisha mwaka 1943. Kisha akafanya kwenye taasisi ya kidini huko Tanta , Zagazig na Alexandria. na baada ya muda mrefu wa uzoefu, Al-Shaarawi alihamia  kwa Saudi Arabia mwaka 1950  kwa kufanya kazi kama profesa wa Sharia katika Umm Al Qura.

Vyeo alivyovishughulisha:

  • Alifanya kuwa mwalimu katika Taasisi ya Tanta Al-Azhari , kisha katika Taasisi ya Alexandria na Taasisi ya Zagazig.
  • Aliajiriwa kufanya kazi huko Saudi Arabia mwaka wa 1950. Na alifanya kazi kama mwalimu katika Kitivo cha Sharia, Chuo Kikuu cha King Abdul Aziz huko Jeddah.
  • Alichaguliwa kama mwakilishi wa Taasisi ya Tanta ya Azhari mnamo 1960.
  • Mteule aliyechaguliwa wito wa Kiislam katika Wizara ya Awqaf mwaka wa 1961.
  • Mtaalamu wa taaluma za Kiarabu katika Al-Azhar Al-Sharif mwaka wa 1962.
  • Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Grand Imam Al-Azhar Sheikh Hassan Mamoun 1964.
  • Alichaguliwa mkuu wa ujumbe wa Al-Azhar nchini Algeria mwaka wa 1966.
  • Alichaguliwa Profesa wa Kutembelea Chuo Kikuu cha King Abdulaziz, Kitivo cha Sharia, Makkah, 1970.
  • Mteule Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Uzamili, Chuo Kikuu cha King Abdul Aziz, 1972.
  • Aliyechaguliwa Waziri wa Mambo ya Awqaf na Al-Azhar katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mwaka wa 1976.
  • Alichaguliwa kama mwanachama wa Kituo cha Utafiti wa Kiislamu mwaka 1980.
  • Alichaguliwa kama mwanachama wa Baraza la halmshuri la Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mwaka 1980.
  • Aliwasilishwa na sheikh wa Al-Azhar pamoja na nafasi katika idadi kadhaa ya nchi za Kiislamu lakini alikataa na akaamua kujitoa kwa wito wa Kiislamu.

"Mohamed Metwally Al- Shaarawi"

Tuzo alizozipata:

  • Imamu Al-Shaarawi alipokea nishani ya daraja la kwanza wakati wa staafisha katika tarehe 15 Aprili 1976 kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Dini (Al-Awqaf)na Al-Azhar.
  • Alipata nishani ya daraja la kwanza mwaka 1983 , Na nishani katika siku ya wahubiri.
  • Alipata Dokta ya heshima katika fasihi kutoka Vyuo vikuu vya Mansoura na Menoufia.
  • Ligi ya Ulimwengu ya Kiislamu huko Makkah ilimchagua kuwa mjumbe wa Kamati ya Uanzishaji wa Mkutano wa Miradi ya Sayansi katika Qur’ani Tukufu na Sunnah, iliyoandaliwa na Chama, na kumpa amri ya kuteuliwa katika taaluma mbalimbali za kisheria na kisayansi. Kutathmini utafiti zilizopatikana katika Mkutano.
  • Mkoa  wa Dakahlia ulimfanya  Al-Shaarawi ni mhusika  wa tamasha la kitamaduni la 1989 linalofanyikwa kila mwaka kumheshimu mmoja wa wana wake maarufu, na lilitangaza mashindano ya kupokea tuzo na himizo, kwa maisha yake na kazi na nafasi yake katika wito wa Kiislamu ndani na nje, na amepewa tuzo kubwa za kifedha.
  • Alichaguliwa na Tuzo la Kimataifa la Qur’an ya Dubai kama Mtu wa Mwaka wa Kiislamu katika kikao chake cha kwanza katika 1418H (1998).

Tungo zake:

Sheikh Al-Shaarawi ana vitabu kadhaa, wengi wa mashabiki wake wamevikusanya na kuandaa kuchapishwa, na kazi maarufu sana hizi na tafsiri kubwa zaidi ya Qurani Tukufu, na vitabu hivi:

  • Mawazo ya Shaarawi.
  • Hadithi za Mitume.
  • Majina ya Mwenyezi Mungu.
  • Wanawake katika Quran Tukufu.
  • Mawazo ya Qurani.
  • Muujiza wa Qurani.
Check Also
Close
Back to top button