Habari

Rais Abdel Fattah El-Sisi aangalia miradi ya Kampuni ya Kiarabu ya Dunia ya Macho katika uwanja wa teknolojia ya macho na elektroniki na matumizi yake katika mifumo ya ulinzi

Ali Mahmoud

Leo, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana na mkuu wa jeshi, Jenerali Tarek Zaghloul, mwenyekiti wa kampuni ya kiarabu ya Dunia ya macho, na Jenerali Tarek Al-Khatib, meneja wa miradi kwenye kampuni hiyo.

Msemaji rasmi wa urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia kuonesha miradi ya kisasa na ya baadaye ya kampuni ya kiarabu ya ulimwenguni ya macho kwa kushirikiana na uzoefu wa ulimwenguni wa muda mrefu katika uwanja wa teknolojia ya macho na elektroniki na matumizi yake katika mifumo ya ulinzi.

Katika muktadha huo, Rais alielekeza kuimarisha juhudi za ujanibishaji wa viwanda na kuhamisha teknolojia ya matumizi katika uwanja wa macho kwa njia inayochangia kutumia kwa malighafi inayopatikana ndani ya nchi, kupunguza uagizaji na kuokoa fedha za kigeni. pia Mheshimiwa Rais alielekeza kuzingatia sekta ya mazoezi na marekebisho ya vitendo na kiufundi na sifa ndani ya mfumo wa ushirikiano na uzoefu wa ulimwenguni wa muda mrefu ili kuandaa kada za binadamu za hali ya juu katika nyanja hizo usahihi na maalumu.

Back to top button