Vijana Na Michezo

Shirikisho la Morocco lamtetea nyota wa “Simba wa Atlas” kuhusu tabia yake katika Kombe la Dunia Qatar

Ali Mahmoud

0:00

Shirikisho la Soka la Morocco lilikabiliana na mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Zakaria Abu Khlal, mchezaji wa “Simba wa Atlas”, ambayo yalimpata kuhusu tabia yake, wakati wa ushiriki wake na timu ya kitaifa ya nchi yake katika Kombe la Dunia “Qatar 2022”.

Tovuti moja ilidai kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akijitahidi, wakati wa uwepo wake katika kambi ya timu ya taifa ya nchi yake huko Qatar “kuvutia idadi kubwa ya wafuasi kwa mwelekeo wake na uvutano wa kidini anaofuata”, na “kuwasukuma kuwa na mawazo yake na kuwaita kwake”.

Shirikisho la Soka la Morocco lilitoa taarifa rasmi kupitia tovuti yake rasmi, ambayo lilimtetea mshambuliaji Abu Khlal, likitishia kuchukua hatua za kisheria, na taarifa hiyo ilisema: “Kufuatia kuchapishwa kwa moja ya tovuti makala inayogusa haiba na tabia ya mchezaji wa kimataifa wa Morocco Zakaria Abu khlal wakati wa ushiriki wake na wachezaji wenzake wa timu ya kitaifa katika fainali za Kombe la Dunia la Qatar 2022..Chuo Kikuu cha Soka cha Kifalme cha Morocoo kilikanusha kabisa madai ya uongo dhidi yake katika makala hiyo”.

taarifa hiyo iliongeza: “Mchezaji huyo alionesha Mwenendo mzuri pamoja na wenzake ili kupata matokeo ya heshima kwa timu ya kitaifa katika Sherehe hiyo ya ulimwengu”.

Iliendelea: “Chuo Kikuu cha Soka cha Kifalme cha Morocco kinaelezea shutuma yake kali za matumizi mabaya ya tovuti hii na mtu na tabia ya mchezaji Zakaria Abu Khlal na kupitia kwake kwa sura ya timu ya taifa na shughuli zake zote”.

Taarifa hiyo ilihitimisha: “pia inathibitisha kwamba itatumia hatua za kisheria kulinda washiriki wa timu ya taifa ya soka na kukanusha madai yote ya uongo yanayoathiri tabia zao au maisha yao binafsi wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kitaifa”.

Mchezaji huyo na wenzake hapo awali walikuwa wamekabiliwa na shutuma kama hizo na kituo cha televisheni cha ujerumani “Welt”, baada ya kuunganisha katika ripoti yake kati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Morocco na kundi la ISIS, kwa sababu ya jinsi walivyosherehekea ushindi wao dhidi ya Ureno katika robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Zakaria Abu Khlal, pamoja na wenzake katika timu ya “Simba wa Atlas”, walichangia kufikia mafanikio ya kihistoria katika mashindano ya Kombe la Dunia la Qatar, na kufikia mraba wa dhahabu kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia.

Back to top button