HabariSiasa

Rais El-Sisi akipewa maelezo na Waziri wa Makazi juu ya matokeo ya ziara ya mwisho ya ujumbe wa mawaziri wa Misri nchini Tanzania kuhusu Bwawa la Julius Nyerere

Ali Mahmoud

0:00

Leo, “Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana na Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, na Dkt. Assem El-Jazzar, Waziri wa Makazi, miundombinu na jamii za mijini”.

Msemaji rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia “kuonesha matokeo ya ziara ya mwisho ya ujumbe wa mawaziri wa Misri nchini Tanzania, pamoja na msimamo wa kiutendaji wa miradi ya kitaifa ya Wizara ya Makazi katika ngazi ya Jamhuri”.

Dkt. Assem El-Jazzar ameonesha matokeo ya ziara ya ujumbe wa mawaziri wa Misri hivi karibuni nchini Tanzania; kushiriki katika maadhimisho ya ujazaji wa kwanza wa Hifadhi ya Bwawa la Julius Nyerere kuzalisha nishati, linalotekelezwa na Muungano wa Misri wa makampuni ya “Makandarasi wa Kiarabu “na” Al-Sewedy Electric”, ambapo bwawa hilo ni mradi mkubwa zaidi wa maendeleo unaotekelezwa nchini Tanzania na utachangia kuzalisha mara mbili ya kiasi cha nishati kinachopatikana sasa nchini, kwa uwezo wa kuhifadhi karibu billioni 34 mita za ujazo, na uwezo wa 2115 megawatt.

Msemaji rasmi aliongeza kuwa mkutano pia ulishughulikia kuonesha hali ya miradi ndani ya mji mkuu mpya wa utawala, haswa hali ya biashara katika vitongoji mbalimbali vya makazi, eneo la pesa na biashara, pamoja na kazi za uratibu wa viwanja na sehemu za barabara, na kazi katika eneo la Green River.

Katika suala hilo, Rais alielekeza utoaji wa vitengo vya makazi kwa kiwango cha punguzo linalofaa wafanyakazi wanaohamia kufanya kazi katika mji mkuu mpya wa utawala, katika miradi ya makazi ya starehe katika eneo la Makazi R3, na ndani ya mfumo wa vifurushi vya fedha vinavyochochea vinavyotolewa na serikali kwa wafanyakazi wa sekta ya serikali katika Mji Mkuu wa Utawala.

Waziri wa nyumba pia alionesha maendeleo ya kazi katika Mji Mpya wa Al-Alamein, ikiwa ni pamoja na miradi kama vile minara, mji wa urithi, Eneo la Kilatini, eneo la burudani, barabara na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Sayansi na teknolojia cha Al-Alamein.

Pia, Rais alipewa taarifa kuhusu maendeleo ya kazi kwa idadi ya miradi ya kitaifa katika Jamhuri, ikiwa ni pamoja na mradi wa “Mgeuko-umbo juu ya nchi ya amani” kwenye Sinai katika maeneo ya Mlima wa Musa na Mlima wa St. Catherine, ambayo ni pamoja na mfululizo wa miradi kamili ya maendeleo, ambapo Mheshimiwa Rais alielekeza kwa makini na maelezo yote ya utendaji ya mradi yawe sambamba na tabia na hadhi ya mahali hapo patakatifu pa nchi ya Misri, na kuwasilisha kwa ubinadamu na kwa wageni wote kutoka Duniani kote kwa njia bora, kuthamini thamani yake ya kipekee ya kiroho.

Rais alifuatilia pia miradi inayoendelea kuendeleza eneo la kihistoria la Kairo, linalolenga kurejesha sura nzuri ya kiustaarabu ya Kairo, ikiwa ni pamoja na mchakato wa maendeleo unaoendelea katika eneo la ukuta wa kijiti cha El-Ayoun na eneo la Pembetatu ya Maspero, pamoja na hatua mpya za utekelezaji wa mradi wa “Kijia cha Watu wa Misri” kwenye kingo za Mto Nile, kuanzia Daraja la Imbaba hadi Daraja la Tahia Misr kaskazini, na kutoka Daraja la Mei 15 hadi Daraja la Qasr El-Nile kusini.

Dkt. Assem Al-Jazzar pia aliwasilisha juhudi zinazofanywa na Wizara ya nyumba kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali zinazohusika kuwahamisha wakazi katika mradi wa Zohour Mei kama makazi mbadala kwa wale walioathirika na mafuriko katika eneo la 15 Mei.

Pia, Rais alipewa taarifa juu ya hali ya pesa ya Mamlaka mpya ya Jamii za mijini, utaratibu wa ugawaji wa ardhi, pamoja na maono ya maendeleo ya mamlaka kupitia miaka kumi ijayo.

Back to top button