
Salwa Al-Mawafi, Balozi wa Misri huko Jamhuri ya Zimbabwe, alikutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri na Waziri wa Afya wa Zimbabwe, Dkt. Constantino Chwenga, aliyesifu urafiki wa kihistoria kati ya Misri na Zimbabwe, Alionesha kuendelea kuimarishwa kwa mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kisiasa kwa kuamsha mahusiano ya kiuchumi, kibiashara na uwekezaji na kufufua kazi ya kamati ya pamoja kati ya nchi hizo mbili.
Makamu wa Rais wa Zimbabwe na Waziri wa Afya alitoa wito kwa makampuni ya Misri kujihusisha zaidi katika sekta ya afya, kilimo, madini na ujenzi katika nchi yake,akiitoa Shukrani kwa serikali ya Misri kwa msaada wake endelevu kwa Zimbabwe katika nyanja za mafunzo, kujenga uwezo na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali.
Kwa upande wake, Balozi wa Misri amethibitisha uungaji mkono endelevu wa Misri kwa ndugu zake wote Barani Afrika, zikiongozwa na Zimbabwe, akiangazia uwazi wa Kairo kwa ushirikiano zaidi na mipango inayofanikisha mema na maendeleo kwa watu wa nchi hizo mbili.
Pia alimshukuru Makamu wa Rais na Waziri wa Afya wa Zimbabwe kwa hamu yake ya kukuza mahusiano ya nchi hizo mbili katika ngazi zote, akiashiria dhamira ya ubalozi mjini Harare kufanya kazi kama kitovu cha uratibu kati ya mashirika mbalimbali ya serikali na taasisi za sekta binafsi kati ya Misri na Zimbabwe na kuimarisha Viunganishi vilivyopo kati yao.