HabariHabari Tofauti

“Wizara ya Mazingira” yashiriki katika Tamasha la kimataifa la kwanza la Port Said la kuwatazama ndege na kuwapiga picha

Ali Mahmoud

0:00

Wizara ya Mazingira ilishiriki katika Tamasha la Kimataifa la Port Said la kuwatazama Ndege na kuwapiga picha katika toleo lake la kwanza, lililofanyika katika Hifadhi ya Ashtom Al-Gameel na Ziwa la Al-Manzala, lililoandaliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ikiwakilishwa na tume ya umma ya Misri ya kukuza Utalii kwa kushirikiana na wizara hilo, Mkoa wa Port Said, Shirika la Ulinzi wa Asili la Misri, na Shirika la Wataalamu wa upigaji picha wa wanyamapori la Misri.

Dkt. Yasmin Fouad alieleza kuwa Tamasha hilo linalenga kukuza utalii wa mazingira katika Mkoa wa Port Said, haswa utalii wa kuwaangalia ndege, kuwatazama na kuwapiga picha kama moja ya aina za utalii wa kimataifa, ambao hupokea watu wengi sana kutoka kwa Wapenda-asili na wapiga picha Nchini Misri na duniani kote, ambapo Misri ni njia muhimu ya pili kwa uhamiaji wa ndege Duniani.

 

“Waziri wa Mazingira” aliongeza kuwa Tamasha la kimataifa la Port Said la kuwatazama ndege na kuwapiga picha litafanyika katika kipindi cha kuanzia 21 hadi 25 Desemba hii, ambapo shughuli za upigaji-picha zilifanyika katika Hifadhi ya Ashtom Al-Gameel na Ziwa la Al-Al-Manzala katika Siku ya Ijumaa, Desemba 23, na ushiriki wa wanafunzi 200 kutoka kwa wapenda kuwatazama ndege na kuwapiga picha.

“Fouad” alisisitiza kuwa suala la kuwalinda ndege wahamiaji na utofauti-tofauti wa kibayolojia ni moja ya changamoto za mazingira za kimataifa na kikanda ambapo Misri kuhakikisha kuzishughulikia wakati wa Mkutano wa Hali ya Hewa COP27 kama moja ya masuala ambayo huonesha kiwango cha mshikamano katika kufikia uwiano kati ya mikataba ya mazingira, ikiwakilishwa katika utekelezaji wa mkataba wa utofauti-tofauti wa kibayolojia utekelezaji wa mpango wa michango ya kitaifa ya serikali katika kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa, na kupunguza uzalishaji. Pia ilijadiliwa kupitia Siku ya utofauti-tofauti wa kibayolojia kwenye mkutano huo, ambayo ilijumuisha kujadili madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kwenye utofauti-tofauti wa kibayolojia mbinu za ulinzi wake katika ngazi ya kimataifa.

Waziri wa Mazingira alisisitiza kuwa kushughulikia kwa Misri katika suala la kuwalinda ndege wanaohama sio tu katika ngazi rasmi au ya kiserikali, lakini pia kulipanua kujumuisha washirika wote kutoka kwa jamii ya kiraia na ya ndani, makampuni ya utalii na vijana …. na mengine, akiashiria kuwa Wizara imeandaa mafunzo mengi ya kujulisha na kuwashirikisha wahusika wote katika ulinzi wa mazingira, ikiwa ni pamoja na: Kuandaa mafunzo maalum kwa wahitimu katika uwanja wa ufuatiliaji ndege wanaohama na kuwatazama, pamoja na mafunzo ya wafanyakazi katika uwanja wa utalii na makampuni, na hata yalienea kwa ushirikishaji wa pointi ya kuwatazama ndege katika Sharm El-Sheikh kama moja ya vivutio vya utalii ambavyo makampuni yaviweka ndani ya mipango yao ya utalii.

“Fouad” alielezea Uzoefu wa Misri katika kuwalinda ndege wa baharini wanaohama katika moja ya njia muhimu zaidi za uhamiaji nchini Misri, ambazo ziliwakilishwa katika mambo kadhaa nayo ni nishati kupitia kuchukua hatua zote za kufunga kwa ombi na mafunzo na ujenzi wa makada wa kitaifa.

Pia kuandaa na kujenga mfumo kamili wa takataka kuwalinda ndege katika njia zao, pamoja na kuidhinisha na kuchukua hatua zote za kuwalinda ndege kutoka katika uwindaji mbali na hayo, kazi inaendelea kukuza ulinzi wa ndege na kujenga utamaduni wa kuwatazama ndege kama moja ya mipango ya utalii wa mazingira na kuunda bidhaa ya utalii inayolingana na kuwatazama ndege wanaohama katika Bahari Nyekundu.

Inatajwa kwamba Ziwa la Manzala na Hifadhi ya Ashtom Al-Gameel ziko na zaidi ya aina 200 za ndege wanaoishi au wanaohama, na maziwa ya kaskazini ya Misri na Mto Nile huzingatiwa miongoni mwa ardhi kubwa na muhimu zaidi zenye unyevu katika Afrika Kaskazini, zinawakilisha asilimia 25 % ya ardhi zenye unyevu katika bonde la Bahari ya Mediterania kwa sababu ndege wa majini wanaohama hupata chakula cha lazima kwake, usalama na mapumziko katika nchi hizi.

Back to top button