Habari

Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Masuala ya Wamisri nje akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania

 

Mnamo Jumapili, Agosti 11, Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Masuala ya Wamisri huko nje Dkt. Badr Abdel Aty, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bw.Mahmoud Thabet Kombo, pembezoni mwa ziara yake ya sasa katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje na Uhamiaji, alieleza kuwa mkutano huo ulijadili mahusiano kati ya pande hizo mbili, ambapo Waziri Abdel Aty alikuwa na nia ya kufikisha salamu za Rais wa Jamhuri kwa Rais wa Tanzania, akielezea nia yake ya kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili, kuongeza kubadilishana biashara, na kushinikiza uwekezaji wa pamoja, kwa manufaa ya watu wawili ndugu.

Msemaji huyo aliongeza kuwa Dkt. Abdel Aty aligusia miradi ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hususani mradi wa Bwawa la Julius Nyerere ambapo alieleza azma ya Misri ya kuondokana na vikwazo vyovyote vinavyoweza kukabili mradi huu, ili kufikia maslahi ya watanzania ndugu. Pia alimwalika mwenzake wa Tanzania kutembelea Misri hivi karibuni.

Back to top button