Misri yatoa msaada wa vidonge 1,400 kwa Djibouti kuchangia sensa ya jumla ya watu

Balozi Khaled El-Shazly, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Djibouti, alikabidhi vidonge 1,400 vilivyotengenezwa na Shirika la Kiarabu la Maendeleo ya Viwanda kwa Wizara ya Uchumi na Fedha ya Djibouti, ndani ya muktadha wa uratibu kati ya Wizara ya Mipango na Maendeleo ya Kiuchumi kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Tume ya Uchumi na Jamii ya Umoja wa Mataifa kwa Asia Magharibi (ESCWA) kushirikiana na Djibouti kutekeleza mradi wa tatu wa sensa nchini Djibouti kwa mwaka 2024.
Balozi wa Misri alisema kuwa mafanikio ya Djibouti katika kuandaa sensa ya jumla ya idadi ya watu yatachangia kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Djibouti, kwani takwimu zitakazotokana na utafiti huo zitakuwa muhimu sana kuwezesha mamlaka ya Djibouti kutekeleza mipango kabambe ya maendeleo kwa misingi ya kisayansi, na kwamba maslahi ya serikali ya Djibouti katika kufanya sensa hii inathibitisha uzito wake katika kutekeleza mipango na sera zilizowekwa, na kwamba Misri inafurahi kuwa na jukumu la kusaidia katika utekelezaji wa kazi hii muhimu.
Kwa upande wake, Waziri wa Uchumi na Fedha wa Djibouti Elias Moussa Douala alielezea kufurahishwa kwake na hatua ya Misri ya kutoa mahitaji ya nchi yake ya vidonge vya kielektroniki na anatarajia ushirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili, hasa katika nyanja za mipango na maendeleo ya kiuchumi.










