Habari

KITUO CHA AFYA MZIHA KUANZA KUTOA HUDUMA JAN,29

0:00

 

 

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI  Dkt. Rashid Mfaume ameagiza Kituo cha Afya Mziha kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuanza kutoa huduma Januari 29, 2024 kutokana na ujenzi wake kukamilika.

Akizungumza Januari 27, 2024  kwenye ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Mvomero na Kituo cha Afya Mziha mkoani Morogoro, Dkt.Mfaume amesema majengo yote yamekamilika likiwamo jengo la OPD, maabara, jengo la upasuaji, jengo la mama na mtoto na kichomea taka na baadhi ya vifaa na vifaatiba vipo na watumishi wapo.

“Watumishi wa afya hakikisheni mnafanya kazi na kutimiza majukumu yenu ya  kuwahudumia wananchi, majengo haya yaendana na utoaji wa huduma bora kwa wananchi muwahudumie kwa lugha nzuri,” amesema.

Aidha Dkt. Mfaume amekemea tabia zinazofanywa na  baadhi ya watumishi  ambazo sio nzuri akieleza Serikali inajenga nyumba za watumishi karibu na hospitali ili kurahisisha utoaji wa huduma  lakini inapotea dharura ya mgonjwa mtumishi  anapohitajika kutoa  huduma  wakati mwingine  hutoa  lugha sio nzuri na hukataa kutoa huduma.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mziha Mhe.Adam Haule na Mkazi wa eneo hilo, Anna Chengula wameishukuru Serikali kwa Kuwajengea kituo hicho ambacho kitapunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuwa kabla ya kituo hicho wajawazito walilazimika kutembea  takribani kilomita 60 kufuata huduma za afya.

Back to top button