Habari
WALIMU WALIOKALIA MADFTARI WAPATA VITI

0:00
Shule ya Msingi Nyansalala iliyoko kata ha Bukondo Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina Jumla ya walimu 12 wakike 6 na wakiume 6.
2.katika Ofisi ya Walimu kulikua na upungufu wa viti na meza za walimu ambapo hivi karibuni walionekana walimu hao kukalia madaftati wanapofanya kazi zao.
Kamati ya shule kwa kutambua changamoto ya uhaba wa meza na viti Kwa ajili ya walimu, ilikaa na kufikia maamuzi ya Kutengeneza viti 8 na meza 8 kupitia Ruzuku ya Serikali ya uendeshaji wa shule (Capitation grants)ili walimu waweze kupata meza na viti vya kwa ajili ya kazi zao.
Viti 8 na meza 8 tayari vipo tayari shuleni Kwa kwa ajili ya MATUMIZI.
Tunatoa pole kwa walimu wetu kwa usumbufu uliojitokeza na kazi iendelee!.