Vijana Na Michezo

RAIS DKT.MWINYI AHIMIZA UMUHIMU WA MAZOEZI

0:00

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza viongozi na wananchi kufanya mazoezi ili kulinda afya na kujikinga na maradhi yasiyoyambukiza kutenga muda wa siku tatu kwa wiki angalau dakika thelathini.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika Tamasha la Mazoezi ya Viungo kitaifa lililoshirikisha Vilabu  149 kutoka Unguja, Pemba na Tanzania Bara kwa matembezi yaliyoanzia Mnarani Kisonge mpaka Uwanja wa Amaan Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 01 Januari 2024

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amehamasisha jamii kushiriki mazoezi na michezo kuepuka na vitendo viovu na magonjwa mbalimbali yasiyoyambukiza.

Back to top button