Habari

ENG MATIVILA AMTAKA MKANDARASI SOKO LA KARIAKOO KUONGEZA KASI YA UJENZI

0:00

 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais TAMISEMI Eng. Rogatius Mativila amemtaka Mkandarasi anayejenga na kukarabati soko la Kariakoo kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo ili  taratibu za kuwarejesha wafanyabiashara zikamilishwe.

Eng. Mativila ametoa kauli hiyo call mara baada ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo jijini Dar es Salaam tarehe 30 Oktoba,2023.

“Amesema mradi wa ukarabati na ujenzi wa Soko hili ni muhimu kwa wafanyabiashara wa Dar ea salaam na mpaka sasa wengi wanahangaika na kujibanza maeneo ambayo sio rafiki kwa biashara hivyo ni vyema Mkandarasi ukaongeza kasi ya ujenzi wa soko hili ili wafanyabiashara wetu wapate nafasi za kufanya biashara katika mazingira ya kisasa ” alisema Eng. Mativila.

Aidha Eng. Mativila amemshkuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha shilingi Bilioni 28.3 zilizofanikisha ujenzi  na ukarabati wa soko hilo ikiwa ni lengo la kuwajali wananchi wapate eneo bora na la kisasa la kufanyia biashara .

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Sigsibert Valentine amesema ujenzi wa Soko hilo umefikia asilimia 91 na  litachukua wafanyabiashara 3500 na maandalizi ya kuwerejesha wafanyabiashara sokoni  yanaendelea.

Mradi huo unatekelezwa kufuatia janga la moto lililotolea Julai 10, 2021 ambapo serikali imetoa shilingi Bilioni 28.03  kufanikisha ujenzi na ukarabati ulioanza Januari 2022 na ulitarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu kupitia mkandarasi Estim  Construction Limited ya Dar es Salaam na mtaalam mshauri akiwa ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Back to top button