RAIS DK.MWINYI ASEMA LENGO LAVUKWA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 umepitiliza ahadi kwa kuvuka lengo kwa miradi ya maendeleo ya huduma za jamii liyopangwa kutekelezwa ikiwemo sekta ya elimu kujengwa kwa Skuli za kisasa Msingi na Sekondari za ghorofa, sekta ya afya kukalimika kwa hospitali za Wilaya na kujenga hospitali za Mikoa, miradi ya maji, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa wanananchi , ujenzi wa barabara za mijini na vijijini, ujenzi wa bandari, ongezeko la mishahara ya wafanyakazi pamoja na ongezeko la pensheni kwa wastaafu na jamii.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Mkoa wa Mjini Magharibi aliweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za ZSSF Tomondo viwanja vya magereza , mradi wa nyumba za gharama nafuu ZHC Mji wa Dk.Hussein Mwinyi Mombasa kwa mchina wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Pia aliweka jiwe la msingi Skuli ya Sekondari ya Mtopepo Wilaya ya Magharibi A na jiwe la msingi Skuli ya Mwembeladu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.










