RC CHALAMILA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI NA MATENGENEZO YA BARABARA TARURA-DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 12, 2023 ameshuhudia utiaji Saini wa mikataba ya kazi za ujenzi na matengenezo ya Barabara TARURA Mkoa wa Dar es Salaam yenye thamani ya Tshs.21,260,364,932.43 katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa DMDP Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiongea wakati wa hafla hiyo amewapongeza wakandarasi walioshinda zabuni ambapo amewataka kufanya kazi kwa Ubora, kuzingatia muda na thamani ya fedha ” Ukipata kazi kafanye kazi kati ya tabia ambayo si itaki ni ya janja janja” Alisema *RC Chalamila*
Aidha RC Chalamila amesema Mhe Rais Dkt Samia amekua akitoa pesa nyingi katika miradi mingi ya maendeleo na ndio maana huwa nasema Ukimvaa Rais Samia Nitakuvaa sina maana ya kupiga ngumi maana yangu hapo ni kuwaonyesha maendeleo yaliyofanywa na Mhe Rais Dkt Samia katika nyanja tofauti hususani wale wanaojifanya hawaoni.
Vilevile RC Chalamila amewataka wakandarasi kutumia fursa za Mabenki na Bima katika kutekeleza majukumu yao ndio maana wataalam wa maeneo hayo wamealikwa katika hafla hii.
Kwa upande wa Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Godfrey Mkinga amesema katika awamu hii ya kwanza TARURA Mkoa ilitangaza Zabuni 57 zenye thamani ya Tshs 24,423,844,249.59 sawa na 60% ya bajeti hadi kufikia Septemba 05, 2023 TARURA imekamilisha michakato ya ununuzi kwa zabuni 53 zenye thamani ya Tshs 21,260,364,932.43 ambazo mikataba yake inatiwa Saini leo, mikataba hiyo inatekelezwa katika Wilaya za Kinondoni, Ubungo, Temeke, Kigamboni na Ilala.