Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA SERIKALI KUTEKELEZA MIPANGO YA KUWASAIDIA VIJANA NA WANAWAKE KWA KILIMO BIASHARA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alisema  Serikali ya Tanzania pamoja na washirika wa maendeleo kwa pamoja wameandaa mikakati shirikishi na kutekeleza mipango mbalimbali ya kusaidia vijana na wanawake  kujishughulisha na kilimo biashara.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo jana tarehe 07 Septemba 2023 akizungumza katika mkutano unaoendelea wa Jukwaa la mifumo ya chakula Afrika unaofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

 

Aidha , Rais Dk.Mwinyi alieleza kuwa ushirikishwaji wa vijana na wanawake katika kilimo na uvuvi unatoa fursa nyingi katika kuendeleza uchumi unaotegemea kilimo vijijini.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amesema mkutano huu unalenga kuhamasisha washirika  wa maendeleo kusaidia mpango wa  BBT wa Tanzania kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana na wanawake katika mifumo ya chakula.

Back to top button