Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YA MWAKA 2023/24 NI MARA MBILI YA FEDHA ZA UVIKO-19

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi leo ameshuhudia hafla fupi ya utiaji saini fedha za mkopo kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 470 kati ya Ofisi ya Rais Wizara ya Fedha na Mipango zilizotolewa na benki ya NBC kwa kushirikiana na benki ya NMB iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.

Rais Dk.Mwinyi amesema fedha za mkopo zitatumika kutekeleza huduma za kijamii ikiwemo sekta ya elimu, afya, barabara, maji, miundombinu sekta ya michezo, ujenzi wa ofisi za Serikali, ujenzi wa Mahakama na miradi mingineyo ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka huu wa fedha wa 2023/24 ni mara mbili kuliko ile ya fedha za miradi ya Uviko-19 na Serikali imejipanga vema.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Abdullla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla, Mawaziri, Makatibu wakuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt.Mwinyi Talib Haji, Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Taifa ya Biashara(NBC ) Theobald Sabi , Afisa mkuu wa fedha benki ya (NMB) Juma Kimori, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa , Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama na Viongozi wa dini.

Back to top button