Habari

Taasisi ya Taaluma za Kidiplomasia yapokea Mkuu wa Shirika la Ford la Marekani

Tasneem Mohammed

Taasisi ya Taaluma za Kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nje ilimpokea Bw. Darren Walker, Mkuu wa Shirika la Ford la Marekani, ambaye kwa sasa anatembelea Kairo.

Aidha, Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya kidiplomasia, Balozi Walid Hajaj, alifanya hafla kubwa ya kumkaribisha Mkuu wa Shirika hilo na kujadiliana naye kuhusu njia za kuimarisha mahusiano ya ushirikiano kati ya Taasisi na Shirika hilo.Balozi Dkt. Hazim Fahm, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje kwa Masuala ya Marekani, Balozi Omar Selim, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mahusiano ya kiutamaduni, na Balozi Dkt. Mohamed El Badry, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Masuala ya Afrika, na kundi la mabalozi na wanadiplomasia wengine ambao hapo awali wote walinufaika na programu za ushirikiano kati ya Taasisi na Shirika la Ford pamoja na Bi.Saba Al-Mobslat, Mkurugenzi wa kikanda wa Shirika la Ford mjini Kairo, na ujumbe unaoandamana unaohusiana na Mkuu wa Shirika hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Balozi Walid Hajaj, alimkaribisha Mkuu wa Shirika hilo na kuupongeza mahusiano pekee ya ushirikiano yanayoendelea kuhusiana kati ya Taasisi na Shirika hilo yanayoanza kwa zaidi ya miongo mitatu na yanyozingatia mchango wa Shirika hilo katika programu na shughuli za kila mwaka zilizoandaliwa na Taasisi ya kujenga uwezo wa viambatanisho Wamisri wa kidiplomasia, hasa kwa kuwatuma katika ziara za mafunzo za nje kwa Marekani, zinajumuisha Washinton na New York.

Pia, aliupongeza urejesho mkubwa wa programu na shughuli hizo, ambazo zilichangia kwa miaka mingi ili kuboresha ujuzi wa makundi mfululizo ya viambatisho wa kidiplomasia na kuwakilisha nguzo ya msingi katika mitaala ya mafunzo inayojumuishwa, inayotekelezwa na Taasisi kwa wanadiplomasia wapya waliojiunga na Wizara ya Mambo ya Nje.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Ford alieleza fahari ya Shirika hilo katika mahusiano ya ushirikiano yanayoungana na Taasisi hiyo, akiashiria kuwa yanawakilisha moja ya nguzo muhimu za kundi la shughuli linalotekelezwa na Shirika hilo nchini Misri, na akiongeza kuwa wanatarajia kukamilisha mpango wa sasa wa ushirikiano kati ya Shirika na Taasisi, unaojumuisha kipindi cha 2022 hadi 2024 na kisha kujenga na kuendelea kufanya upya kwa njia inayoingia katika jitihada zinazotolewa za kutoa mafunzo na kujenga uwezo wa vijana wanadiplomasia wa Misri.

Back to top button