RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA GAVANA MAO WA JIMBO LA HUNAN CHINA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Hussein Ali Mwinyi amesema ushiriki wa Tanzania katika Mkutano mkuu wa Tatu wa China na Afrika umeimarisha zaidi uhusiano wa watu bara hilo na China.
Ameyasema hayo leo alipokutana na Gavana wa Jimbo la Hunan, mjini Changsha hapa China Mheshimiwa Mao Weiming kwa mazungumzo. Jimbo la Hunan ndipo alipozaliwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China Marehemu Mao Tse Tung.
Dk Mwinyi amesifu kazi kubwa ya utabibu inayofanywa na jimbo la Hunan katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Ameonesha matumaini yake kwamba ushirikiano huo utazidi kuimarika.
Kwa upande wake Gavana Mao ametaka uhusiano uzidi kuimarishwa katika nyanja nyingine ikiwemo biashara.