Waziri Mkuu apokea Waziri Mkuu wa India na ujumbe ulioandamana katika Uwanja wa Ndege wa Kairo
Mervet Sakr
Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, leo Jumamosi Juni 24 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kairo, alimpokea Bw. Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India, anayetembelea Misri kwa ziara ya kiserikali, kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Ujumbe ulioambatana na Waziri Mkuu wa India ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Mshauri wa Usalama wa Taifa, na maafisa kadhaa waandamizi wa Baraza la Mawaziri na Wizara ya Mambo ya Nje ya India.
Sherehe rasmi ya kuwakaribisha wageni wa India katika uwanja wa ndege wa Kairo.
Mawaziri wakuu wa Misri na India wanatarajiwa kufanya mazungumzo leo katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri, kwa mahudhurio ya mawaziri kadhaa na maafisa kutoka pande zote mbili, kujadili masuala ya ushirikiano kati ya Misri na India.