Vijana Na Michezo

MICHUANO YA SOKA WANAWAKE YAFIKIA NUSU FAINALI – UMISSETA 2023

Timu za Soka Wasichana kutoka Mikoa ya Dodoma, Manyara, Mbeya na Tabora zimeingia nusu fainali katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Mkoani Tabora.

Michezo ya Robo Fainali imepigwa Tarehe 22 Juni 2023 kwenye viwanja A na Uwanja Mpya shule ya Sekondari Tabora wavulana, ambapo mchezo wa kwanza Mbeya iliifunga Kagera 3-0.

Mchezo mwingine wa robo fainali ulizikutanisha majirani Arusha na Manyara ukimalizika kwa Manyara kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na baadae wenyeji Tabora kuifunga Mara kwa penati 6-5 baada ya kwenda sare ya 1-1 kwenye muda wa kawaida.

Katika mchezo wa mwisho uwanja A kati ya Dodoma na Dar es salaam, mikwaju ya penati ililazimika kutumika ili kumpata mshindi baada ya timu zote kutoshana nguvu ya 0-0 kwenye muda wa kawaida na Dodoma kusonga mbele kwa penati 4-3.

Kwa matokeo haya sasa michezo ya nusu fainali itazikutanisha Manyara vs Tabora na vijana wa Makao Makuu ya Nchi Dodoma watakutana na Mbeya kasha watapatikana washindi wawili watakaokutana kwenye fainali inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi Tarehe 24 Juni 2023.

Back to top button