Uchumi

Waziri wa Fedha akutana na mwenzake wa Kenya

Mervet Sakr

Dkt. Mohamed Maait, Waziri wa Fedha, alifanya mkutano wa nchi mbili na mwenzake wa Kenya, Ngoguna Ndungo, pembezoni mwa ushiriki wao katika mikutano ya Benki ya Afrika ya Mauzo ya Nje na Uagizaji  (AFREXIMBANK) nchini Ghana.

Pande hizo mbili zilijadili hali ya uchumi wa Dunia na athari zake kwa uchumi wa Afrika na changamoto wanazozipata ili kuendelea kukuza mchakato wa maendeleo.

Pande hizo mbili zimekaribisha kuimarishwa kwa mahusiano ya pamoja wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kuhimiza sekta binafsi ya nchi hizo mbili kutafuta fursa zaidi za kuanzisha uwekezaji wa pamoja ili kutumia rasilimali zinazofurahiwa na nchi hizo mbili, pamoja na kujadili njia za kuhamasisha matumizi ya sarafu za kitaifa kutatua mabadilishano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Pande hizo mbili zilijadili njia za kukabiliana na mshtuko wa kiuchumi wa nje, na kushughulikia vyema na kwa urahisi na matokeo ya mgogoro wa sasa wa ulimwengu, na athari zake mbaya kwa uchumi wa Afrika, ndani ya muktadha wa juhudi za pamoja kufikia maoni ya Umoja na ufumbuzi wa haraka ili kupunguza athari mbaya za mshtuko wa nje kwenye bajeti za nchi za Afrika, kwa kufanya kazi ili kuongeza juhudi za ushirikiano wa kiuchumi wa Afrika, kufikia maendeleo endelevu, ikionyesha kuwa COMESA ni moja ya kambi za kikanda zilizofanikiwa zaidi Barani Afrika zinazolenga kufikia ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi wanachama.

Waziri huyo alimwalika mwenzake wa Kenya kuhudhuria mkutano wa uzinduzi wa Muungano wa Madeni kwa Maendeleo Endelevu nchini Misri, Septemba ijayo.

Back to top button