Habari

Rais El-Sisi akutana na mwenzake wa Malawi

Mervet Sakr

0:00

Leo, Rais Abdel Fattah El-Sisi amekutana na Rais Lazarus Chakwera wa Jamhuri ya Malawi, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa COMESA katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Msemaji Rasmi wa Urais wa Misri, Mshauri Ahmed Fahmy, alisema kuwa Rais alithibitisha fahari ya Misri katika mahusiano ya pamoja kati ya Misri na Malawi, akisifu kwa suala hili jukumu la Malawi katika kanda ya Kusini mwa Afrika, na kuonesha nia ya Misri kufanya kazi ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili nndugu katika nyanja mbalimbali, hasa uwekezaji, kubadilishana biashara na kujenga uwezo kwa makada wa Malawi.

Kwa upande wake, Rais wa Malawi alithamini maendeleo endelevu mnamo kipindi cha mahusiano ya nchi mbili kati ya Misri na Malawi, akielezea shukrani kubwa ya nchi yake kwa Misri, watu wake na uongozi, na kwa jukumu lake la upainia katika kuongoza gurudumu la hatua za pamoja za Afrika, akisisitiza kuwepo kwa matarajio mapana ya kuendeleza mahusiano na kuendeleza mifumo ya ushirikiano wa nchi mbili kati ya nchi hizo mbili ndugu katika nyanja mbalimbali za maendeleo na kiufundi.

Msemaji huyo aliongeza kuwa marais hao wawili walijadili maendeleo katika masuala kadhaa ya kikanda na mafaili ya Afrika, ambapo walikubaliana katika suala hili kuendelea na uratibu baina ya nchi hizo mbili kuhusu masuala ya usalama na utulivu na kufikia malengo ya maendeleo katika ngazi ya bara la Afrika, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika suala hilo kupitia uanachama wa pamoja wa nchi hizo mbili katika ngazi ya Umoja wa Afrika na kundi la COMESA.

Back to top button