Habari

MAMA MARIAM MWINYI: “FANYENI MAZOEZI,KULENI VYAKULA VYENYE VIRUTUBISHO”

0:00

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa jamii kuzingatia suala  la  Usalama wa Chakula kwani maradhi yatokanayo na chakula yamekuwa yakiongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula ambavyo si salama kusababisha kuathiri afya  za wananchi.

Ameyasema hayo leo  tarehe 07 Juni 2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Usalama wa Chakula Duniani yaliyoanza kwa matembezi  ya kilomita tano kuanzia  Ofisi za Makao makuu ya  ZFDA Mombasa hadi Mapinduzi Square (Kisonge), Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Mama Mariam amesema  kula vyakula  vyenye virutubisho, kilicho safi  ni mtindo bora wa kula pamoja na kufanya mazoezi ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kutibu maradhi  mbalimbali yatokanayo na mlo usiotimia.

Vilevile kwa kuzingatia kula  mlo uliotimia  wenye makundi maalumu ya vyakula bora ikiwemo mbogamboga, matunda, kunde, karanga, mbegumbegu , jamii ya wanyama na mazao ya baharini, nafaka , mzizi , ndizi mbichi na mafuta  kwa afya bora  kwa Watoto, Wazee na Wajawazito  ili kuimarisha  na kuweka mfumo imara wa kinga mwilini.

Back to top button