Habari

RAIS DK.MWINYI AHUDHURIA JUKWAA LA UCHUMI QATAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo tarehe: 23 Mei 2023 amehudhuria ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi

ambapo viongozi mbalimbali duniani wamehudhuria ufunguzi huo akiwemo Rais wa Rwanda Paul Kagame.

Kabla ya ufunguzi wa Jukwaa hilo Dk. Mwinyi alizungumza na Mhe. Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Amir wa Taifa la Qatar.

Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Qatar hutumia Jukwaa hilo la biashara kila mwaka kujitangaza kiuchumi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali.

Back to top button