Habari

Dk.Hussein Mwinyi akutana na viongozi wa kampuni ya Power International Holding

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika mwendelezo wa ziara yake nchini Qatar, amekutana na viongozi wa kampuni ya Power International Holding. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wameonesha kupendezwa na mradi wa umeme wa Zanzibar, kuashiria fursa kubwa za uwekezaji katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya Zanzibar.

Katika hatua nyingine ya ziara yake, Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Abu Issa Holding, Bw. Ashraf Abu Issa, kampuni inayojihusisha na uwakala wa usafirishaji watalii. Katika mazungumzo yao, Rais Dk. Mwinyi ametoa wito kwa kampuni hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya watalii Zanzibar na pia kuwashawishi wawekezaji wengine kuja kuwekeza katika visiwa vidogo vidogo vilivyopo Zanzibar.

Kesho Jumanne, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kushiriki katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi mjini Doha. Mkutano huu mkubwa utahudhuriwa na viongozi kadhaa wa dunia, akiwemo Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Back to top button