Wizara ya Vijana na Michezo na Chuo cha Mpira wa Mikono cha Afrika zatekeleza kozi ya mafunzo kwa makocha wa Afrika kwa leseni za kimataifa
Mervet Sakr
Shughuli za kozi ya tatu ya mafunzo kwa makocha wa Afrika kupata leseni ya kimataifa “B”, inayotekelezwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika na Chuo cha Mpira wa Mikono cha Afrika, itakayofanyika kuanzia Mei 13 hadi 19, ilianza jana katika Ukumbi wa Dkt. Hassan Mustafa huko eneo la Oktoba sita.
Ambapo Wizara ya Vijana na Michezo, ikiwakilishwa na Idara kuu ya Utendaji wa Michezo, “Utawala Mkuu wa Maandalizi ya Makada na Viongozi wa Michezo”, iliyoratibiwa na Shirikisho la Afrika na Chuo cha Mpira wa Mikono cha Afrika ili kujua maandalizi ya mwisho ya utekelezaji kwa suala la (tarehe za kuwasili na kuondoka kwa makocha – malazi na kujikimu – kumbi za mihadhara – viwanja vya michezo na zana za mafunzo), kulingana na itifaki iliyosainiwa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la Mpira wa Mikono la Afrika, inayolenga kusaidia shughuli za kisayansi za Chuo cha Mpira wa Mikono cha Afrika.
Naye Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy amesisitiza nia yake ya dhati ya ushirikiano baina ya Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la Mpira wa Mikono Afrika ili kuendeleza michezo na kukuza mpira wa mikono Barani Afrika haswa baada ya uamuzi wa Umoja wa Afrika kuwa kuanzia mwaka 2024, hakuna kocha atakayeruhusiwa kusajiliwa katika orodha ya timu zitakazoshiriki mechi isipokuwa zile ambazo zimepata leseni mbalimbali za Shirikisho la Kimataifa kulingana na viwango vya mashindano.
Hivyo, Wizara hiyo ilikuwa makini katika ushirikiano wake kusaidia kuandaa kozi ya mafunzo ili kuendeleza kiwango cha makocha na kuwapatia leseni mbalimbali za kimataifa zinazonufaisha maendeleo ya mpira wa mikono Barani Afrika, na kuongeza kuwa idadi ya washiriki katika kozi hiyo ilifikia makocha “23” kutoka nchi 8 za Afrika.
Ikumbukwe kuwa kozi ya kwanza ya mafunzo ilifanyika mwaka 2019 kwa kushirikisha wakufunzi 50 kutoka nchi nyingi za bara la Afrika kupata leseni (D) na kozi ya pili ya mafunzo ilifanyika mwaka 2021 ili kupata leseni (C)