Habari Tofauti

DK.MWINYI AMESEMA SERIKALI IMEANZA KUAJIRI WAUGUZI NA MADAKTARI ZNZ

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeanza kuajiri Wauguzi na imeongeza nafasi  za ajira kwa madaktari  na watumishi wengine wa sekta ya afya.

Ameyasema hayo leo katika Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imefanya jitihada kubwa kwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya, kujenga miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali za Wilaya na Mkoa pamoja na vituo vya afya Unguja na Pemba.

Vilevile, Serikali imeendelea na juhudi katika ununuzi wa vifaa vya tiba na uchunguzi..

Back to top button