Habari

RAIS DK.MWINYI APOKEA RIPOTI YA CAG ZANZIBAR

0:00

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dk.Othman Abass Ali Ikulu , Zanzibar.

Akipokea ripoti hiyo Rais Dk.Mwinyi amemuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba , Sheria , Utumishi na Utawala Bora kuiwasilisha katika Baraza la Wawakilishi.

Kifungu cha 112(5) kinamtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali awasilishe taarifa yote aliyoikagua na akabidhi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa hatua nyengine.

Back to top button