Habari Tofauti
Jumuiya ya Kiarabu yasaidia Nchi za Afrika kwa Kozi za Mafunzo katika Umwagiliaji na Uzalishaji wa Wanyama
Mervet Sakr
Jumanne, asubuhi,Mfuko wa Nchi za Kiarabu kwa Msaada wa Kiufundi kwa Nchi za Afrika wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu ulianzisha kozi mbili za mafunzo kwa wahandisi 50 wa kilimo katika Jamhuri ya Burundi, mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 10 hadi 16 Aprili 2023 katika nyanja za mbinu za kisasa za umwagiliaji na uzalishaji wa wanyama, na mafunzo hayo yanajumuisha upande wa nadharia na vitendo.
Naibu wa kwanza wa Waziri wa Kilimo wa Burundi alieleza uangalifu unaotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Burundi kwa sekta ya kilimo na maendeleo yake ili kukuza uchumi, akisisitiza nia ya Wizara yake kuendeleza ushirikiano huo ili kujumuisha sekta nyingine.