Habari

DKT.MWINYI AFUTARI NA WAZEE,WALEMAVU YATIMA , PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI WA MKOA WA KUSINI PEMBA

Ahmed Hassan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DkT. Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi amejumuika na Wananchi kutoka makundi ya watu wenye ulemavu, yatima, Wazee na viongozi wa dini kwenye sala na futari aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba leo tarehe 11 Aprili, 2023 Uwanja wa kufurahishia watoto Tibirinzi.
Aidha, Rais Alhaj DkT.Mwinyi amesema tangu kuanza kwa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan mzunguko wa kufutari na wananchi ulianza kwa Mikoa yote Unguja na leo ameanza Mikoa ya Pemba na kumaliza kesho.
Back to top button