Habari Tofauti
MAMA MARIAM MWINYI AMSHUKURU BALOZI WA CHINA
Leo, Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amemshukuru Balozi mdogo wa China anayefanya kazi zake Zanzibar Mhe.Zhang Zhisheng kwa msaada wa Mabegi ya shule mia moja ambayo ilikuwa ahadi yake aliyotoa tarehe 20 Machi ,2023 wakati wa Maadhimisho ya Mwaka mmoja wa ZMBF .Halfa hiyo imefanyika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani .
Mama Mariam Mwinyi amesema atagawa msaada huo wa mabegi kwa watoto wenye mahitaji maalum katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.