Habari

Rais Abdel Fattah El-Sisi ampokea Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Ali Mahmoud

Rais Abdel Fattah El-Sisi alimpokea Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Sameh Shoukry, Waziri wa Mambo ya Nje, pamoja na Bw. Daniel Rubinstein, Msimamizi wa shughuli za ubalozi wa Marekani jijini Kairo.

Msemaji rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa Mheshimiwa Rais alielezea furaha yake ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, akiwasilisha salamu zake kwa Rais “Joe Biden”, na akisisitiza mahusiano ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Misri na Marekani, na kuangalia mbele kwa kuongeza uratibu na mashauriano kati ya pande hizo mbili kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na usalama na masuala ya eneo.

Kwa upande wake, “Blinken” aliwasilisha salamu za Rais wa Marekani kwa Mheshimiwa Rais, akisisitiza kuwa ndani ya mfumo wa mahusiano ya kimkakati kati ya nchi hizo mbili rafiki, Washington inategemea uratibu mkubwa na Misri chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais kurejesha uthabiti, kufikia utulivu na kudhibiti hali kati ya Pande za Palestina na Israeli, na mzungumzaji rasmi alieleza kuwa katika muktadha huu, maendeleo na matukio ya hivi karibuni katika Maeneo ya Palestina, juhudi za pamoja na shughuli za Misri zinazoendelea kudhibiti mvutano unaoongezeka kupitia siku zilizopita, ambapo Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa maendeleo ya matukio ya hivi karibuni yanathibitisha umuhimu wa kufanya kazi mara moja katika mfumo wa njia za kisiasa na kiusalama ili kutuliza hali na kupunguza kuchukua hatua zozote zo upande mmoja kutoka kwa pande hizo mbili, akisisitiza msimamo thabiti wa Misri wa kufikia suluhisho la haki na la kina linalohakikisha haki za watu wa Palestina kwa mujibu wa marejeleo ya kimataifa, na kwa njia ambayo inatatua suala hilo muhimu katika eneo na kufungua matarajio ya amani, utulivu, ushirikiano na ujenzi.

Msemaji rasmi aliongeza kuwa wakati wa mkutano huo, maoni na mitazamo yalibadilishana juu ya masuala kadhaa ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi ya pamoja, mbali na mada kadhaa za uhusiano wa nchi mbili kati ya pande hizo mbili.

Katika muktadha huu, suala la Bwawa la Renaissance lilishughulikiwa, ambapo Mheshimiwa Rais alisisitiza msimamo thabiti Wa Misri katika suala hili kupitia hitaji la kufikia makubaliano ya kisheria ya kujaza na kuendesha Bwawa, kwa njia ambayo hufikia masilahi ya pamoja na kuhifadhi haki za maji na maendeleo ya pande zote, akisisitiza umuhimu wa jukumu kubwa la Marekani katika kutatua mgogoro huo.

Back to top button