Vijana Na Michezo

Vijana na Michezo yaonesha Shughuli zake ndani ya Matukio ya Siku ya Kwanza ya Toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo

Mrevet Sakr

Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy imeendelea kuonesha shughuli na programu zake ndani ya matukio ya siku ya kwanza ya toleo la 54 la Maonesho ya Kimataifa ya Kitabu ya Kairo, ambayo Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu ameyafungua katika kituo cha Maonesho huko The Fifith Settlement, yatakayoendelea hadi Februari 6, 2023, pamoja na uangalizi wa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mheshimiwa Abdel Fattah El-Sisi.

Hiyo inakuja ndani ya mfumo wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Wizara ya Utamaduni katika ngazi zote.

Matukio hayo yana kauli mbiu “Kwa jina la Misri – Pamoja: Twasoma… Twafikiri…Twaunda.” ambapo kupitia Idara Kuu ya Wachanga Wizara iliandaa warsha mbalimbali kuhusu ” Sanaa ya uandishi wa Hadithi fupi kwa ushirikiano wa Bi. Hasnat Al-Hakim, Mkurugenzi wa Uhariri_ katika Gazeti la Al-Akhbar, na Mchoraji Ahmed Abdel – Aleem_ katika Gazeti la Al- Akhbar, warsha nyingine ya “Caricature” ya Msanii Nesma Ashraf, na warsha ya “Vifaa” ya Msanii Rana Hatem.

Kulingana na muktadha huo, Idara kuu kwa Kuwawezesha Vijana umefanya” Vikao vya Mazungumzo” chini ya kichwa” Boresha na Badilisha”, pia warsha ya vilabu vya hali ya hewa, ambayo imeendeshwa na kikundi mashuhuri cha wakufunzi na waratibu wa vilabu vya hali ya hewa katika Wizara.

Vilevile Wizara imeandaa idadi ya mikutano ya uelewa masuala ya kijamii, katika ukumbi wa sanaa wa Al-Azhar, kwa ushirikiano wa Al-Azhar Al-Shareif, pamoja na uwepo wa Sheikh Ahmed Makki- Mtangazaji wa programu “Viongozi wa Fikra”, Sheikh Ahmed Hammam, na Sheikh Hassan Azzam kutoka kwa wanachuoni wa Al-Azhar.

Na Wizara ina nia ya kukuza uelewa na ujuzi kwa wachanga na vijana, na kuunga mkono na kuendeleza uwezo wao. Banda la Wizara ya Vijana na Michezo limejumuisha vitabu vya programu muhimu zaidi zilizotekelezwa ndani ya wizara, Maonesho ya nyaraka za miradi mbalimbali ya Wizara” Maendeleo ya Wachanga _ Maendeleo ya Michezo _ Maendeleo ya Vijana_ Uwezeshaji Vijana _ Elimu ya Uraia _ Miji kwa Vijana_ Vituo vya Vijana na programu ” Rayhana” na timu ya “Kayani”.

Back to top button