Rais El-Sisi afuatilia juhudi za kuyalinda makundi yaliyo hatarini zaidi ya yatima, watoto na vijana wasio na huduma za kifamilia
Ali Mahmoud
Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alikutana, Jumamosi, na Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri mkuu, na Bi. Nevin Al-Qabbaj, Waziri wa Mshikamano wa Kijamii”.
Msemaji rasmi wa Urais wa Jamhuri alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia “ufuatiliaji wa mipango ya kulinda makundi yaliyo hatarini zaidi, haswa yatima na watoto wasio na huduma za familia”.
Mheshimiwa Rais aliagiza kuharakisha kukamilika kwa muswada wa sheria ya matunzo mbadala, inayotoa njia zote za ulinzi kwa makundi yaliyo hatarini zaidi, akisisitiza umuhimu wa kuwa mamlaka zote husika kutoka katika Wizara na vyama vya kiraia kuzingatia juhudi zao katika kutoa njia zote za huduma kutoa msaada na ulinzi jumuishi kwa watoto yatima, kuongeza uwezo wao na kuukuza, na kuendeleza huduma za kitaasisi na kifamilia zinazotolewa kwao kutoa mazingira ya jamii yenye afya kwa malezi yao.
Mheshimiwa Rais pia aliagiza kutoa nyanja zote za msaada kusaidia haki za watu wenye mahitaji maalum katika nyanja zote za maisha, kama vile ujumuishaji wa jamii, taasisi za elimu, kazi na usafirishaji, mheshimiwa Rais akiagiza, katika suala hili, kudhamini mipango miwili iliyozinduliwa na Wizara ya Mshikamano wa Jamii kando ya mkutano wa “Qaderoon Bikhtilaf”, nao ni mpango wa “Upatikanaji” kutoa mazingira na teknolojia zinazohitajika kuwezesha mawasiliano ya watu wenye mahitaji maalum na pembe zote na huduma za jamii, pamoja na mpango wa “Rafiki Bora zlZaidi” unaolenga kukomesha kutengwa kijamii na kiuchumi kwa watu wenye mahitaji maalum.
Kuhusu mwenendo wa serikali kuelekea uwekaji kidijitali na utayarishaji wa hifadhidata zote, Mheshimiwa Rais aliagiza uzinduzi wa jukwaa la kielektroniki la wadaiwa na madeni wa kiume na wa kike pamoja na kuliunganisha kimitandao na taasisi zote zinazohusika za vyama vya kiraia zinazofanya kazi katika uwanja huu, kusaidia jukwaa kuharakisha kufanya utafiti wa kijamii kwa wadaiwa na madeni, na kuchunguza njia bora za kutibu sababu za faini.
Msemaji rasmi huyo aliongeza kuwa Bi. Waziri wa Mshikamano wa Jamii pia alipitia juhudi za wizara kwa ajili ya matunzo ya familia kupitia mfululizo wa mipango jumuishi unaolenga kuimarisha thamani ya familia, kusaidia jukumu lake na kusaidia wanachama wake wote kufikia uwezeshaji wa kiuchumi na kijamii, pamoja na kulinda makundi yaliyo hatarini katika familia kutoka kwa yatima, wazee au watu wenye mahitaji maalum, pamoja na kutoa njia zote zinazowezekana za ulinzi wa jamii kuwaepusha hali za maisha ya kulazimishwa yanayoathiri nafsi yao na mwingiliano wao na jamii.