Siasa

Balozi wa Misri nchini Sudan Kusini akutana na Waziri wa Uwekezaji

Ali Mahmoud

Balozi Moataz Mustafa Abdel Kader, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Sudan Kusini, alikutana na Waziri wa Uwekezaji “Dhieu Matouk”, ambapo mkutano huo ulishughulikia njia za kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na biashara kati ya nchi hizo mbili, na changamoto zinazowakabili wawekezaji katika nchi hizo mbili.

Wakati wa mkutano huo, Balozi wa Misri alisisitiza nguvu na uimara wa mahusiano ya milele na ya kihistoria kati ya nchi mbili za kidugu, akionesha maendeleo mazuri katika mwendo wa mahusiano ya nchi mbili katika nyanja zote, na akisisitiza umuhimu wa kujulikana na kuoneshwa mahusiano hayo katika sekta za uwekezaji na biashara kwa namna ambayo inakidhi mahitaji ya watu wa nchi hizo wa kidugu kwa kuzingatia mgogoro wa kiuchumi Duniani, na kufikia ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Waziri “Matouk” alisisitiza fahari ya nchi yake kwa mahusiano ya kihistoria na mashuhuri na watu na uongozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na msaada unaotolewa kwao. Pia alionesha matarajio ya uwekezaji nchini Sudan Kusini, akiangazia maeneo mbalimbali ya kuahidi ambayo yatafanikisha ukuaji wa kiuchumi nchini mwake.

Mkutano huo pia ulishughulikia mifumo ya kisheria inayosimamia ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, na dhamana mbalimbali zinazotolewa kwa wawekezaji. Pande hizo mbili zilijadiliana mipango inayohitajiwa kufanya toleo la pili la maonesho ya Bidhaa za Misri nchini Sudan Kusini kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana na toleo la kwanza.

Back to top button