Tanzania: Ujenzi Bandari ya Mbamba-Bay kuanza mwezi huu
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari ya Mbamba-Bay mwezi huu.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Plasduce Mbossa amesema mpango ya kujenga bandari kuanzia mwezi huu ulishawekwa na kwamba utaanza kutekelezwa.
“TPA tunatambua umuhimu wa Bandari ya Mbamba Bay na tunatekeleza yote tuliyoahidi, ili kufungua ushoroba wa Kusini na Bandari yetu ya Mtwara,” amesema.
Mbossa ametoa taarifa hiyo kufuatia ombi la Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole ambaye alitaka TPA ijenge haraka Bandari ya Mbamba-Bay, ili Mtwara iweze kufunguka zaidi kuichumi.
“Ili Mtwara kama mkoa na wilaya ifunguke ni lazima ushoroba wa Mtwara ufunguke upande wa pili wa ushoroba ambapo ni Bandari ya Mbamba-Bay,” alisema.
Amesema Bandari ya Mtwara, ndiyo kituo cha cha kuondokea mizigo inayoingia na kutoka Mtwara na kama haifanyi kazi itakuwa vigumu kwa Bandari ya Mtwara kutumika ipasavyo.
“Tusifurahie tu kwamba Bandari ya Mtwara iko vizur kama Bandari ya Mtwara ya Mbamba Bay, ambayo ndiyo point ya pili ya kuondokea mizigo inayoingia Mtwara haifanyi kazi,” amesema.
Polepole amesema itakuwa ni vigumu meli zinazopeleka mizigo Zambia, Malawi na Msumbiji kwenda Bandari ya Mtwara bila kujengwa Bandari ya Mbamba Bay.