Habari

Waziri wa Mambo ya Nje akutana na mwenzake wa Tanzania

 

Ijumaa Januari 19, Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukry alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Janyori Mkamba, pembezoni mwa Mkutano wa Harakati ya kutofungamana kwa Upande wowote uliofanyika katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Balozi Ahmed Abu Zeid, Msemaji na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje, alisema kuwa mkutano huo ulishughulikia njia za kuimarisha mahusiano kati ya pande hizo mbili, haswa kuhusiana na hali ya uchumi na kazi ya kuongeza viwango vya ubadilishaji wa biashara, kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania alivyoelezea kuridhishwa kwake na kuongezeka kwa viwango vya uwekezaji wa Misri nchini mwake mnamo kipindi cha mwisho.

Msemaji huyo aliongeza kuwa mkutano huo pia umegusia maendeleo ya hivi karibuni yanayohusiana na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kuhusu ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere na maandalizi yanayoendelea ya kusherehekea uendeshaji wa awali wa bwawa hilo, pamoja na toleo lijalo la kamati ya pamoja kati ya nchi hizo mbili, iliyopangwa kufanyika Tanzania mwaka huu.

Balozi Abou Zeid alihitimisha hotuba yake akibainisha kuwa pande hizo mbili zilikubaliana kuendelea na mashauriano ya njia za kuendeleza mahusiano ya nchi hizo mbili, ambapo Waziri Shoukry alielezea kukaribisha kwake kwa mwenzake wa Tanzania mjini Kairo mapema iwezekanavyo.

Back to top button