Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ufuatiliaji wa mahusiano ya Misri – Afrika
Ndani ya muktadha wa mikutano yake ya mara kwa mara katika Wizara ya Mambo ya Nje kuratibu juhudi za kitaifa za kuimarisha na kuendeleza ushirikiano na nchi za Afrika, Kamati ya Kudumu ya Ufuatiliaji wa mahusiano ua Misri na Afrika ilifanya mkutano asubuhi ya Oktoba 24, iliyoongozwa na Balozi Hamdi Sanad Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Mambo ya Afrika, na kwa ushiriki wa maafisa waandamizi kutoka wizara husika na Chama cha Wasafirishaji wa Misri.
Mkutano huo ulipitia ripoti zilizopokelewa kutoka kwa Balozi za Misri katika nchi za Afrika kuhusu maendeleo ya kubadilishana biashara na uwepo wa makampuni ya Misri ndani yao, na maandalizi yanayoendelea kwa Misri kuwa mwenyeji wa Maonyesho ya Biashara ya Ndani ya Afrika 2023 katika kipindi cha kuanzia 9-15 Novemba 2023 kwa usimamizi wa Benki ya Usafirishaji wa Nje ya Afrika na kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika.
Mkutano huo pia ulishughulikia mafanikio yaliyopatikana katika kusafirisha dawa za Misri kwa baadhi ya nchi za Afrika na jinsi ya kuijenga na kuipanua katika hatua inayofuata, pamoja na uzoefu wa nchi kadhaa katika kufanya biashara ya kubadilishana kupitia mikataba sawa au kutegemea sarafu za ndani kuzifadhili.