Habari

ZANZIBAR ILIANZISHA MPANGO WA UWEKEZAJI WA SEKTA YA MAJI 2022-2027

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ilianzisha mpango wa uwekezaji maji wa mwaka 2022 hadi 2027 uliolenga kukusanya rasilimali kwa ajili ya uwekezaji salama wa maji kwa utekelezaji endelevu wa muda mrefu wa usambazaji maji kwa mahitaji ya msingi na kiuchumi.

Rais Dk Mwinyi amesema hayo leo tarehe 25 Oktoba 2023 alipofungua kongamano la 24 la maji linaloshirikisha mataifa kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa mpango huo umezingatia maeneo matano yakiwemo uwekezaji wa maji na fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za maji na usafi wa mazingira, kujenga uwezo wa kuhimili hali hewa, usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kijamii, kuimarisha utaratibu wa kitaasisi pamoja na uchumi wa buluu na usimamizi endelevu wa rasilimali maji.

Back to top button