Habari

Julius Kambarage Nyerere

Utaifa wa kiafrika bila ya Umoja wa kiafrika wa kweli utakuwa bure, mwenye hatari, na umepitwa na wakati”

Ile ni kauli ya rais mtanzania “Julius Nyerere” kama ilitajwa kwenye kitabu cha” Robert Emerson- kwa Umoja wa kiafrika”, katika mwaka wa 2009.

“Julius Kambrake Nyerere “,mwenye lakabu ya baba wa Taifa”, alizaliwa katika mwezi wa Machi, mwaka wa 1922, katika kabila la “Zanki”, kwenye kijiji cha”Butyama”, kutoka familia ya kabila linalofanya kazi ya Ufugaji, na baba yake ni kiongozi wake, alikufa mwezi wa Oktoba, mwaka wa 1999, kama ni baba kwa wavulana watano na wasichana wawili, alijulikana kwa Uaminifu na Uongozi, aliitwa kwa” Mwalimu”, na “Mwanafunzi wa nchi yake na Mwalimu wake.

Alifanya kazi ya kufundisha baaya ya kupata shahada ya pili Uingereza, kisha akaanzisha chama cha “TANU” kwa lengo la ukomboa wa amani kutoka kwa sera ya ukoloni -inayowahimiza viongozi wa kikabila-kuwakilishwa katika sera ya ubaguzi na kutengwa. Mwaka 1961, akawa Waziri Mkuu wa Tanganyika baada ya kupata uhuru wake, na kisha miaka miwili baadaye Zanzibar ikapata uhuru wake pia, na alitangaza umoja wake na Tanganyika chini ya jina la dola (Tanzania) mwaka uliofuata wa 1964, na kumteua “Nyerere” kuwa rais wake, kisha kwa kuachia urais mwaka 1985.

Ni mmoja wa watetezi wakuu wa umoja wa Afrika,na mmoja wa waanzilishi wa harakati za kuikomboa kutoka kwa ukoloni katika miaka ya sitini na sabini, ni mmoja wa waasisi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika – Umoja wa Afrika sasa – ulioanzishwa mwaka mmoja baada ya mapendekezo ya (Mkutano wa Addis Ababa) Mei 1962, ambapo alisema: “Tunaamini katika umoja wa Afrika, tukiamini Afrika yenyewe.

Inatajwa kwa Uongozi wake uliendelea kwa vipindi vinne vya Urais, mnamo vyake alipata Uungaji mikono, Upendo, na Usaidizi kutokana na nchi yake, hasa matabaka ya maarufu, na hayo kwa sababu ya kuwa na mtindo wa “Ujamaa “, na kwa maoni yake, Ujamaa ni mchanganyiko wa” Ujamaa wa kiutendaji” na “Ukomunisti wa kiafrika”, pia katika mwaka wa 1992, aliruhusu kufanya marekebisho ya Katiba nchini wake;ili nchi yake ipitishe mifumo ya vyama vingi vya siasa.Na mnamo mwaka 1967, Tanzania iliingia katika Muungano wa nchi tatu za mashariki ya Afrika ulioitwa ( Umoja wa mashariki ya Afrika), na aliifanya lugha ya Kiswahili lugha rasmi ya nchi zake, na kupitia hayo, aliweza kuondoa tofauti hizo na kupunguza ukali wa tofauti katika makabila ya mashariki na katikati ya Afrika.

Alikuwa msomi, anayependa Fasihi ya Ulimwengu, alifasiri kwa lugha ya Kiswahili ( Mfanyabiashara wa Bunduki), (Julius Kaisar) kwa Shekespeer, pia ana vitabu vingi navyo ni kama:  Uhuru na Umoja 1967, Uhuru na Ujamaa 1968, Uhuru na Maendeleo 1973. Linalosisitiza juu ya Imani yake kubwa kwa Ujamaa wa kiafrika na kwamba Elimu iwe kwa wote, nayo ni njia ya kuikomboa watu wa nchi.

Alikuwa na Urafiki adhimu sana pamoja na rais mmisri aliyekufa” Gamal Abd Elnaser “, kulingana na mradi wake nchini Tanzania unaofanana na mradi wa “Nasser ” nchini Miari ambapo wote walibeba nembo ya “Ujamaa” na wao waliangalia mielekeo ya pamoja inayohusu masuala ya bara la Afrika na Masuala ya kitaifa, na mnamo mwaka wa 1964 Bwana “Salem Ahmed Salem” aliainishwa kama Balozi wa kwanza kwa Tanzania nchini Misri, wakati wa Umoja kati ya Tanganika na Zanzibar.

Na bwana Nasser katika hotuba zake nchini Misri, alimsifu Nyerere kwamba ( yeye ni mwanafunzi wa nchi yake na mwalimu wake, naye ni mmoja wa waafrika adhimu mnamo wakati wake), na mnamo ziara yake kwa Bunge aliisisitiza tena akasema:Nyerere ni kiongozi mgumu, shujaa, na mwaminifu, siyo kwa Tanzania tu wala kwa Afrika bali kwa Utu mzima”, na inatajwa kwamba rais Nyerere alihuzunika sana kwa kifo cha rais mmisri Abd Elnaser, akasema:Kifo cha Abd Elnaser ni msiba mkubwa na hasara kubwa sana kwa Ulimwengu wote, hata maadui wake watamhuzunika, alikuwa mwanamume adhimu, baadaye alilia. Na  ni vyema  kutajwa kuwa, ilikuwa mara ya kwanza ya kulia kwa Nyerere na mtu alimwona.

Back to top button