Habari

RAIS DK.MWINYI ASEMA ZANZIBAR IMENUFAIKA  NA FURSA NYINGI ZA MAENDELEO KUTOKA CHINA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar imenufaika na fursa nyingi kutoka China kupitia sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo afya hususan kupokea timu za madaktari bingwa wanaofika nchini kubadilishana uzoefu na wazawa  katika kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina yao pamoja na kujifunza uzoefu wa masuala mbalimbali ya afya.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 11 Septemba 2023 Ikulu, Zanzibar alipowakabidhi vyeti na medali timu ya madaktari 32 kutoka China waliohudumu kwenye hospitali za Zanzibar kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuwaaga baada ya kumaliza muda wao nchini.

Naye, Kiongozi mkuu wa timu ya madaktari hao 32, Dk.Zhao Xiaojun ameishukuru Serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano ilioutoa kipindi chote na kueleza Zanzibar ni visiwa vyenye upendo, amani na mshikamano kwa wenyeji na wageni.

Back to top button