Habari

NCHI IMEANDIKA HISTORIA KWA KUWAKABIDHI URAIA WA TANZANIA WAHAMIAJI WASIOHAMISHIKA 3,319

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema nchi imeandika historia mpya kwa kuwakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319 ambao wameishi nchini kwa zaidi ya miaka 50 wakiwa na asili ya mataifa jirani ya Burundi, Comoro, Msumbiji na Rwanda.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo leo tarehe 05 Septemba 2023 katika hafla ya kukabidhi vyeti  vya uraia wa Tanzania kundi la Wahamiaji wasiohamishika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amefurahishwa kutekelezwa ahadi yake aliyoitoa baada ya kuingia madarakani mwaka 2020 kwa kumalizika zoezi hilo na kuwafanya watambulike kuwa Raia wa Tanzania  badala ya Wahamiaji wasiohamishika.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji nchini  kuziimarisha sheria zilizopo hususani sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuwa sheria hii haijafanyiwa mapitio kwa kipindi kirefu kwa madhumuni ya kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika nchini.

Back to top button