Habari

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AWASILISHA TAARIFA

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga jana 17/08/2023 aliewasilisha taarifa ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na OMR kwa Mh  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu katika Ofisi za Ikulu Chamwino.

Pamoja na Mazungumzo hayo Bi.Maganga amepata fursa ya kumpatia Mhe. Rais machapisho mbalimbali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwemo kitabu cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – Chimbuko, Misingi na Maendeleo pamoja kitabu cha Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Back to top button