Jumatatu 10/7, Rais Abdel Fattah El-Sisi alipigiwa simu na Rais Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Algeria.
Msemaji rasmi wa Ofisi ya Rais wa Misri, Mshauri Ahmed Fahmy, alisema kuwa simu hiyo iligusia kujadili masuala kadhaa yanayohusiana na uhusiano wa nchi mbili kati ya Misri na Algeria, ndani ya muktadha wa nia ya marais hao wawili kuendelea na juhudi za kupanua na kuimarisha wigo na maeneo mbalimbali ya ushirikiano, kwa njia inayoongeza maslahi ya pamoja ya nchi mbili ndugu na watu wao.
Marais hao wawili pia walibadilishana maoni na mitazamo juu ya masuala ya kikanda na kimataifa ya maslahi ya pamoja, na njia za kushughulikia changamoto zinazokabili eneo hilo, kwa kuzingatia jukumu la nchi hizo mbili na nia yao ya kuongeza hatua za pamoja za Kiarabu.