RIADHA YAFIKIA TAMATI UMISSETA 2023 TABORA

Michezo ya riadha imehitimishwa leo Tarehe 20 Juni 2023, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Mkoani Tabora.
Fainali ya mwisho ya riadha UMISSETA 2023 imefanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondanri Wavulana Tabora, ikihusisha Mita 200, 400, 800 na 1500 kwa Wasichana na Wavulana.
Siwema Julius wa Pwani aliibuka mshindi Mita 200 baada ya kutumia Sekunde 25.66 akifuatiwa na Stumai Msemwa wa Njombe aliyetumia Sekunde 26.03, na nafasi ya tatu kwenda kwa Bertha Adrea wa Kilimanjaro Sekunde 26.16.
Mita 200 Wavulana Matiku Nyamalanga wa Mara aliibuka Bingwa baada ya kukimbia kwa Sekunde 22.80, akifuatiwa na Emmanuel Amos wa Pwani Sekunde 22.92 na mwenzake Kimana Kibase wa Pwani kumaliza wa tatu kwa Sekunde 23.21.
Upande wa Riadha Mita 3000 Wasichana, Nduile Poti wa Pwani uliibuka tena bingwa baada kukimbia kwa dakika 10.26.47 akifuatiwa na Salome Kapera wa Shinyanga dakika 10.37.03 na Lucia Ezekiel wa Arusha akamaliza nafasi ya tatu akitumia dakika 10.38.78.
Mita 3000 Wavulana Ubingwa umeenda Mkoa wa Manyara baada ya Agustino Leonard kutumia dakika 8.45.66, nafasi ya pili nayo ikaenda Manyara kufuatia Jofrey Philipo kukimbia kwa dakika 8.54.81 na Damian Christian wa Arusha kumaliza watatu kwa dakika 8.51.72.
Fainali ya UMISSETA 2023 upande wa riadha imehitimishwa huku wakimbiaji kutoka mikoa mbalimbali wakionesha vipaji vya hali ya juu hali iliyopelekea wadau na makocha wa riadha kutoka maeneo mbalimbali nchini kujitokeza ili kufanya machagua ya vijana kwa ajili ya kuwaendeleza zaidi.