Habari

DK.MWINYI AHITIMISHA ZIARA UNGUJA

0:00

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amehitimisha Ziara yake kwa Mikoa iliyopo Unguja ambayo aliianza mapema mwezi Mei Mkoa wa Magharibi na kuhitimisha leo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika Ziara hiyo Dk.Mwinyi amezungumza na Viongozi wa CCM ngazi ya shina, Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM ngazi ya Jimbo, Wilaya na Mikoa.
Rais Dk. Mwinyi amehitimisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua miradi ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwemo eneo la Kituo cha Mafuta Mahonda, kitega uchumi cha CCM Nungwi, eneo la CCM Afisi kuu Kiwengwa, Shamba la CCM Afisi kuu Kilombero.
Back to top button