Leo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amewasili Dar es Salaam kushiriki na kuongoza akiwa Msarifu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation kikao cha ndani na wadau wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation. Kikao hiki kimelenga kuimarisha uhusiano wa Taasisi hiyo na wadau wake katika kuchangia mipango ya maendeleo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar katika Sekta ya Afya.
Pia jioni atahudhuria dhifa ya kitaifa kwa ajili ya Rais wa Rwanda Paul Kagame iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam.