Habari

Balozi wa Misri akutana na Waziri wa Afya wa Congo

Mervet Sakr

Balozi Hisham Abdel Salam Al-Makoud amekutana na Waziri wa Afya wa Congo Samuel Roger Kamba Mulamba ambapo mkutano huo umejadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja wa matibabu.

Katika mkutano huo, Balozi Hisham Abdel Salam Al-Makoud alisisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Balozi huyo pia alieleza nia ya Misri kupeleka msafara wa matibabu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kutoa baadhi ya huduma za matibabu kwa manufaa ya wananchi wa Congo.

Kwa upande wake, Waziri huyo wa Congo aliahidi kuanza kujiandaa kwa msafara huo, akisifu mahusiano ya kihistoria kati ya Misri na Congo, yanayoshuhudia maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali mnamo kipindi cha hivi karibuni, haswa katika uwanja wa Afya.

Mwishoni mwa mkutano huo, balozi wa Misri alimkabidhi Waziri wa Congo mwaliko wa kuhudhuria Mkutano wa Pili wa Matibabu wa Afrika ‘ Africa Health ExCon” uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 6 hadi 11 Juni 2023 mjini Kairo.

Back to top button