Habari

Sameh Shoukry: Hamna utashi wa Ethiopia wa kufikia makubaliano kuhusu Bwawa la Renaissance (Al-Nahda)

Mervet Sakr

0:00

Waziri wa mambo ya nje Sameh Shoukry ameshasema kuwa: Hamna utashi wa Ethiopia wa kufikia makubaliano kuhusu Bwawa la Renaissance (Al-Nahda).

Hayo yalijiri wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Kenya Alfred Mutua.

Shoukry alidokeza kuwa Misri haikupinga kuutumia Mto Nile kwa ajili ya maendeleo, na nchi za Afrika lazima ziunganishwe ili kufikia maendeleo.

Waziri huyo wa mambo ya nje alisisitiza kuwa makubaliano yoyote kuhusu Bwawa la Renaissance(Al-Nahda) hayapaswi kuzidhuru nchi hizo mbili za chini.

Shoukry aliongeza kuwa Misri iko tayari kufanya kazi ili kufikia uelewa kuhusu mgogoro wa Bwawa la Renaissance.

Waziri huyo wa mambo ya nje alidokeza kuwa Misri imekuwa ikijihusisha katika mazungumzo ya Bwawa la Renaissance kwa miaka 10.

Back to top button