Habari

DKT. MWINYI AMEYATAKA MASHIRIKA YA UMMA KUJITATHIMINI KWA KUFUNGUA UKURASA MPYA WA UFANISI NA UENDESHAJI KWA KULETA TIJA KWA WANANCHI

Ahmed Hassan

0:00

RAIS DKT .MWINYI AMEYATAKA MASHIRIKA YA UMMA KUJITATHIMINI KWA KUFUNGUA UKURASA MPYA WA UFANISI NA UENDESHAJI KWA KULETA TIJA KWA WANANCHI

Rais Dkt. Mwinyi ameyataka mashirika ya umma yanayotoa huduma kwa wananchi kutafuta ufumbuzi wa haraka kutatua changamoto zinazowakabili na kuzigeuza kuwa fursa zenye tija kuleta mabadiliko chanya ikiwemo kubadili mifumo ya taasisi zao inapoonekana inafaa kwa maslahi ya umma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi, aliyasema hayo Ikulu Zanzibar, alipokutana na Watendaji wakuu wa Mashirika hayo na kuwaelekeza kufanya marekebisho na maboresho ya kiutendaji watakapoona mazingira hayapo sawa kwa mustakabali wa mashirika na Serikali kwa ujumla.

Aidha, Dkt.Mwinyi alisema waache utendaji wa kusuasua badala yake wabuni mikakati ya mageuzi yenye kuleta mabadiliko ya haraka kwa kutoa huduma za uhakika kwa wananchi na tija kwa Serikali.

Back to top button